• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 28, 2014

  SALUM ABUBAKAR 'SURE BOY' MCHEZAJI BORA OKTOBA

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa timu ya Azam, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini.
  Abubakar ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) aliwashinda wachezaji wengine 20, huku wanne kati ya hao wakichuana naye kwa karibu.
  Wachezaji hao ni Joseph Mahundi wa Coastal Union, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Najim Magulu wa JKT Ruvu Stars.
  Kwa kuibuka mchezaji bora, Abubakar atazawadiwa kikombe na fedha taslimu Sh. Milioni 1 kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
  Salum Abubakar 'Sure Boy' amekuwa Mchezaji Bora wa Oktoba Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

  Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SALUM ABUBAKAR 'SURE BOY' MCHEZAJI BORA OKTOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top