• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 30, 2014

  TFF YATANGAZA BONGE LA TENDA KWA WABUNIFU, NI DILI LA JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linakaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini. Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.
  Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).
  Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio na Garden Avenue. Mwisho wa kupokea designs ni Novemba 15, 2014.
  Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YATANGAZA BONGE LA TENDA KWA WABUNIFU, NI DILI LA JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top