• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 26, 2014

  MTIBWA SUGAR YAJITANUA KILELENI, YAITADIKA MBEYA CITY 2-0 SOKOINE

  MTIBWA Sugar imeonyesha dhamira ya kutwaa tena ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya jioni ya leo kuilaza mabao 2-0 Mbeya City Uwanja Sokoine mjini Mbeya.
  Ushindi huo unaifanya Mtibwa Sugar itemize pointi 13 baada ya kucheza mechi tano na kujiimarisha kileleni mwa ligi hiyo, ikiwazidi kwa pointi tatu Azam na Yanga,
  Ame Ally aliifungia Mtibwa Sugar bao la kwanza akiunganisha kwa guu la kulia kona iliyochongwa na beki wa zamani wa Yanga, David Luhende na kuwanyong'onyesha wenyeji dakika ya 21.
  Mtokea benchini Vincent Barnabas alikokota mpira hadi kwenye boksi la wenyeji na kumchambua kwa shuti la kitoto lililompita ubavuni kipa bora msimu wa 2012/2013 David Burhan na kuwapa wageni goli la pili dakika ya 76.
  Baada ya kufunga bao hilo, Barnabas na wachezaji wengine wa Mtibwa Sugar walikwenda karibu na jukwaa la mashabiki wa Mbeya City kushangilia, jambo ambalo liliwakera mashabiki hao na kuanza kurusha chupa za maji uwanjani. Kulitokea vurugu kidogo ambazo zilizimwa na Jeshi la Polisi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAJITANUA KILELENI, YAITADIKA MBEYA CITY 2-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top