• HABARI MPYA

    Thursday, October 30, 2014

    MAN CITY WAPIGWA 2-0 ETIHAD KWAO, WAVULIWA UBINGWA NA KUTUPWA NJE KOMBE LA LIGI, NEWCASTLE YATINGA ROBO FAINALI

    KLABU ya Manchester City imevuliwa ubingwa wa Kombe Ligi, kufuatia kuchapwa mabao 2-0 na Newcastle Uwanja wa Etihad ambayo sasa inakwenda Robo Fainali.
    Rolando Aarons alifunga bao la kwanza akimtungua kipa wa tatu, Willy Caballero dakika ya sita kabla ya Moussa Sissoko kufunga la pili dakika ya 75.
    Manchester City sasa inatimiza mechi tatu bila kushinda na mchezo ujao itamenyana na mahasimu wa Jiji, Man United Jumapili.
    Kikosi cha Man City kilikuwa; Caballero, Sagna, Demichelis, Mangala, Kolarov, Fernandinho, Toure/Navas dk59, Milner, Jovetic, Silva/Nasri dk8/Aguero dk69 na Dzeko.
    Newcastle; Elliot, Janmaat/Sissoko dk64, Coloccini, Dummett, Haidara, Abeid, Obertan, Taylor, Colback, Aarons/Ameobi dk45 na Armstrong/Riviere dk64.
    Newcastle imeitoa nje Manchester City michuano ya Capital One Cup baada ya mabao ya Rolando Aarons na Moussa Sissoko (pichani)

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2813230/Manchester-City-0-2-Newcastle-Rolando-Aarons-Moussa-Sissoko-strike-knock-holders-Capital-One-Cup.html#ixzz3HbBNiR8E 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY WAPIGWA 2-0 ETIHAD KWAO, WAVULIWA UBINGWA NA KUTUPWA NJE KOMBE LA LIGI, NEWCASTLE YATINGA ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top