• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 24, 2014

  SPURS YAUA 5-1 ULAYA, ETO'O NA EVERTON WATOKA KAPA UFARANSA

  TOTENHAM Hotspur imeifumua mabao 5-1 Asteras Tripolis ya Ugiriki katika mchezo wa Europa League usiku wa jana Uwanja wa White Hart Lane. 
  Harry Kane alifunga bao la kwanza dakika ya 13, kabla ya Erik Lamela 'Rabona' aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 30 kuongeza la pili dakika ya 29 na la tatu kipindi cha pili.
  Kane akakamilisha hat-trick yake kwa mabao mawili zaidi dakika za 75 na 81, kabla ya kipa wa Tottenham, Hugo Lloris kutolewa kwa kadi nyekundu.
  Kane akaenda kusimama langoni kwa kuwa tayari timu hiyo ilikuwa imekwishakamilisha idadi ya wachezaji watatu wa kubadilisha.
  Mchezaji wa Asteras Tripolis aliyetokea benchi, Jeronimo Barrales alifunga kwa mpira wa adhabu akimtungua Kane, ambaye jitihada zake za kuokoa hazikufanikiwa.
  Samuel Eto'o akiwatoka mabeki wa Lille jana Ufaransa

  Timu nyingine ya England iliyosalia kwenye michuano hiyo, Everton imelazimisha sare ya bila kufungana ugenini dhidi ya Lille ya Ufaransa.

  Hat-trick hero Harry Kane (left) swaps shirts with Hugo Lloris after the Tottenham goalkeeper is sent off in the 87th minute
  Shujaa wa Hat-trick, Harry Kane (kushoto) akichukua jezi ya kipa kwenda kuziba nafasi ya Hugo Lloris aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 87
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SPURS YAUA 5-1 ULAYA, ETO'O NA EVERTON WATOKA KAPA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top