• HABARI MPYA

    Thursday, October 23, 2014

    ATLETICO MADRID YAUA 4-0, JUVE YACHAPWA, MONACO YAAMBULIA SARE

    ATLETICO Madrid imeendeleza moto wake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuichapa mabao 5-0 nyumbani Malmo FF ya Sweden katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Ushindi huo umetokana na mabao ya Koke dakika ya 48, Mandzukic dakika ya 61, Griezmann dakika ya 63, Godin dakika ya 87 na Cerci dakika ya 90 na ushei.  Mchezo mwingine wa kundi hilo, Olympiacos imeshinda 1-0 nyumbani dhidi ya Juventus.
    Katika mechi za Kundi C,  Bayer Leverkusen imeshinda nyumbani mabao 2-0 dhidi ya Zenit St Petersburg wakati Monaco imelazimishwa sare ya 0-0 nyumbani na Benfica.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ATLETICO MADRID YAUA 4-0, JUVE YACHAPWA, MONACO YAAMBULIA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top