Na Mahmoud Zubeiry, MBEYA
KOCHA wa Prisons ya Mbeya, David Mwamwaja amesema anaelekeza nguvu zake katika mchezo ujao dhidi ya Simba SC Oktoba 25, mwaka huu baada ya jana kufungwa na JKT Ruvu.
Prisons jana ilichapwa mabao 2-1 na JKT Ruvu ya Pwani iliyohamishia maskani Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine Mbeya.
Na Jumamosi itaikaribisha Simba SC katika mchezo mwingine wa ligi hiyo kwenye Uwanja huo huo. “Tumekubali matokeo, sasa tunaelekeza nguvu zetu katika mchezo wetu ujao,”alisema Mwamwaja akizungumza na BIN ZUBEIRY jana.
Mwamwaja amesema kwamba mchezo wa jana walipoteza kwa bahati mbaya, kwa sababu walitengeneza nafasi nyingi, lakini wakashindwa kuzitumia.
“Tulitengeneza nafasi nyingi nzuri, lakini kwa bahati mbaya tukashindwa kuzitumia. Wenzetu jana walikuwa wana bahati, walitumia nafasi zao, wakashinda mchezo,”amesema Mwamwaja, aliyewahi kuifundisha Simba SC.
Akizungumzia mchezo na Simba SC Jumamosi, Mwamwaja amesema anatarajia utakuwa mgumu kwa sababu watakutana na timu bora na kongwe.
“Na pia kama unavyojua, Simba SC hawajashinda mechi hata moja msimu huu, wametoa sare zote nne, sasa lazima watataka kuja kushinda hapa, kwa hiyo utakuwa mchezo mgumu na sisi tutajiandaa kikamilifu,”amesema.

![]() |
Kocha wa Prisons, David Mwamwaja amesema anaelekeza nguvu kwenye mechi na Simba SC |
Mwamwaja amesema kwamba mchezo wa jana walipoteza kwa bahati mbaya, kwa sababu walitengeneza nafasi nyingi, lakini wakashindwa kuzitumia.
“Tulitengeneza nafasi nyingi nzuri, lakini kwa bahati mbaya tukashindwa kuzitumia. Wenzetu jana walikuwa wana bahati, walitumia nafasi zao, wakashinda mchezo,”amesema Mwamwaja, aliyewahi kuifundisha Simba SC.
Akizungumzia mchezo na Simba SC Jumamosi, Mwamwaja amesema anatarajia utakuwa mgumu kwa sababu watakutana na timu bora na kongwe.
“Na pia kama unavyojua, Simba SC hawajashinda mechi hata moja msimu huu, wametoa sare zote nne, sasa lazima watataka kuja kushinda hapa, kwa hiyo utakuwa mchezo mgumu na sisi tutajiandaa kikamilifu,”amesema.
0 comments:
Post a Comment