• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 24, 2014

  MOURINHO ASEMA DIEGO COSTA AWEZA CHEZA DHIDI YA MAN UNITED JUMAPILI

  KOCHA Jose Mourinho ameghairi kumuweka benchi mshambuliaji Diego Costa katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United Jumapili.
  Mshambuliaji huyo wa kati wa Hispania, amekosa mechi mbili zilizopita katokana na maumivu ya nyama na wiki hii alipelekwa hospitali kwa tiba ya tatizo hilo.
  Lakini Mourinho, ambaye amethibitisha Loic Remy atakuwa nje kwa wiki tatu zijazo kwa maumivu ya nyonga, amesema mshambuliaji wake huyo nyota ana nafasi ya kwenda Old Trafford.  

  Diego Costa ana nafasi ya kuivaa Manchester United Uwanja wa Old Trafford, amesema kocha wa Chelsea, Jose Mourinho

  Alipoulizwa leo iwapo Costa atacheza, Mourinho akasema: "Kuna nafasi, ana nafasi ndogo. Diego ana nafasi kidogo, sawa na Ramires na (John Obi) Mikel. Lakini Remy yuko nje na hatacheza. Hana nafasi,".
  "Kila kitu kilichotokea (kwa Costa). Alikuwa majeruhi kama kawaida- hiyo ilikuwa ni nyama. Ilibidi aende hospitali kwa matibabu, tatizo ambalo tusingeweza kulitatua bila kuwa hospitali kwa usiku mmoja- hiyo ilikuwa kabla ya kucheza na Maribor,"amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOURINHO ASEMA DIEGO COSTA AWEZA CHEZA DHIDI YA MAN UNITED JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top