• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 25, 2014

  NDANDA FC HALI BADO SI SHWARI, YAFUNGWA MECHI YA NNE MFULULIZO LICHA YA KUFUKUZA MAKOCHA

  Simba SC imetoa sare ya tano mfululizo katika Ligi Kuu leo, wakati Ndanda FC imefungwa mechi ya nne mfululizo

  MATOKEO LEO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA

  Azam FC 0-1 JKT Ruvu
  Prisons 1-1 Simba SC
  Kagera Sugar 1-1 Coastal
  Ruvu Shoot 1-0 Polisi Moro
  Ndanda FC 0-1 Mgambo Stand Utd 0-3 Yanga SC
  HALI imezidi kuwa mbaya kwa Ndanda FC, baada ya leo kufungwa mechi ya nne mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  Bao pekee la Ally Nassor dakika ya tatu, limeipa ushindi wa 1-0 Mgambo JKT dhidi ya Ndanda ambayo iliwafukuza makocha wake, Dennis Kitambi na Muharami Mohamed 'Shilton' baada ya kufungwa 3-1 Jumamosi iliyopita na Ruvu Shooting, tangu ishinde 4-1 dhidi ya Stand United mjini Shinyanga katika mchezo wa kwanza Septemba 21, mwaka huu, Ndanda ikageuka ‘gunia la mazoezi’.
  Mechi nyingine za leo, Ruvu Shooting imeilaza 1-0 Polisi Moro, bao pekee la Zuberi Dabi dakika ya 68 Uwanja wa Mabatini, Chalinze mkoani Pwani, Yanga imeshinda 3-0 Shinyanga dhidi ya Stand United, Simba 1-1 na Prisons mini Mbeya, Kagera Sugar na Coastal Union 1-1 mjini Bukoba na Azam FC imechapwa 1-0 na JKT Ruvu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDANDA FC HALI BADO SI SHWARI, YAFUNGWA MECHI YA NNE MFULULIZO LICHA YA KUFUKUZA MAKOCHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top