• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 25, 2014

  WINGA PRISONS ‘AWATIA HOMA’ SIMBA SC

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC wamepata taarifa kuhusu winga machachari wa Prisons, Hamisi Maingo na wanaonekana kujipanga kikamilifu kwa ajili ya mchezo huo.
  Jina la Maingo limo kwenye orodha ya wachezaji wa kuchunga wa Prisons ya benchi la ufundi la Simba SC, chini ya kocha Mkuu, Patrick Phiri.
  Maingo aliwasumbua mno mabeki wa Yanga SC timu hizo zilipokutana mwezi uliopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Prisons kulala 2-1 kwa mbinde.
  Hamisi Maingo aliyeruka juu dhidi ya beki wa JKT Ruvu, Haruna Shamte

  Akaendelea kuwa tishio pia katika mechi na Azam FC na JKT Ruvu, kiasi kwamba tayari ameingia kwenye orodha ya wachezaji tishio katika Ligi Kuu msimu huu.
  Simba SC inamenyana na Prisons leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya katika mfulullizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WINGA PRISONS ‘AWATIA HOMA’ SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top