• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 25, 2014

  MAN CITY YALALA 2-1 KWA WEST HAM

  MANCHESTER City imechapwa mabao 2-1 na West Ham United jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya England ugenini jioni ya leo.
  Mabao yaliyowazamisha mabingwa hao watetezi yamefungwa na Morgan Amalfitano dakika ya 21 na Diafra Sakho dakika ya 75, wakati bao pekee la City limefungwa na David Silva dakika ya 77.
  Kikosi cha West Ham kilikuwa; Adrian, Jenkinson, Collins, Reid, Cresswell, Song 8, Noble, Amalfitano/Kouyate dk67, Downing, Valencia/Cole dk76 na Sakho/Nolan dk89.
  Manchester City; Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Clichy/Kolarov dk78, Navas, Fernando/Milner dk78, Toure, Silva, Aguero na Dzeko/Jovetic dk59.

  Diafra Sakho akishangilia na Cheikhou Kouyate
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YALALA 2-1 KWA WEST HAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top