• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 29, 2014

  DROGBA AIPELEKA CHELSEA NANE BORA CAPITAL ONE CUP

  KLABU ya Chelsea imetinga Robo Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup baada ya kuichapa mabao 2-1 Shrewsbury usiku huu.
  Chelsea ilipata bao la kwanza mapema tu kipindi wakati mkongwe, Didier Drogba alipomalizia pasi maridadi ya mwanasoka wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah.
  Lakini Shrewsbury ikapata bao la kusawazisha kupitia kwa Andrew Mangan aliyetokea benchi dakika ya 77, kabla ya Jermaine Grandison kujifunga dakika nne baadaye kuipa ushindi timu ya Jose Mourinho.
  Didier Drogba akipongezwa na wenzake baada ya kufunga
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DROGBA AIPELEKA CHELSEA NANE BORA CAPITAL ONE CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top