• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 24, 2014

  DI MARIA YUKO FITI KABISA KUWAVAA CHELSEA JUMAPILI OLD TRAFFORD

  WINGA Angel di Maria yuko fiti kuichezea Manchester United dhidi ya Chelsea Jumapili.
  Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 60 katika klabu hiyo alikuwa alipata maumivu ya mguu United ikitoa sare ya 2-2 na West Bromwich Albion Jumatatu na kulikuwa kuna wasiwasi ataukosa mchezo huo mkubwa zaidi kwa msimu huu hadi sasa.
  Aliwekewa barafu baada ya kutolewa dakika ya 76 Jumatatu, lakini ameweza mkufanya mazoezi kwa siku mbili zilizopita na yuko tayari kwa kipute na Chelsea keshokutwa.

  Angel di Maria akiwa mazoezini na Chris Smalling kujiandaa na mechi dhidi ya vinara wa Ligi Kuu England Chelsea Uwanja wa Old Trafford Jumapili  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DI MARIA YUKO FITI KABISA KUWAVAA CHELSEA JUMAPILI OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top