• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 26, 2014

  RONALDO: MAN UNITED MPENI MUDA VAN GAAL AFANYE MAMBO YAWE MAMBO

  MWANASOKA Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo ametaka kocha Louis van Gaal ape we muda Manchester United, kama Sir Alex Ferguson na ametabiri Mholanzi huyo atarejesha mataji Old Trafford.
  Nyota huyo wa Real Madrid amepanga kutazama mechi kati ya United dhidi ya Chelsea leo Jumapili kupitia Televisheni nchini Hispania na anaamini Angel Di Maria aliye fiti tena atafanua vitu.
  United inazidiwa kwa pointi na Chelsea vinara wa Ligi Kuu ya England hadi sasa, ikiwa imeshinda mechi tatu tu kati nane hadi sasa na Ronaldo anafikiri pengo hilo ni kubwa na kwamba timu ya Jose Mourinho ina nafasi ya ubingwa.

  Cristiano Ronaldo amewaambia Manchester United wampe muda Louis Van Gaal Ronaldo thinks Van Gaal (pictured) can lead United to Premier League and Champions League success
  Ronaldo anafikiri Van Gaal (pichani) anaweza kuipa Untied nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya

  Lakini anafikiri Van Gaal ataiongoza United kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
  "Wakati fulani makocha wanahitaji muda kuzibadilisha timu kwa namna wanavyotaka," amesema Ronaldo. "Katika Ligi Kuu ya England timu zote zinapigania pointi nyingi na hata timu zilizo mkiani kwenye ligi, zinaweza kuzifunga zilizo juu kwenye kilele. Hivyo ni ngumu,".
  "Kupata kikosi kizuri na timu nzuri inachukua muda, hivyo tumpe Van Gaal muda anaouhitaji. Ni kocha babu kubwa na mwenye uzoefu sana na ninaamini ataipa ubingwa tena  United, kama si mwaka huu, basi karibu sana kutoka sasa,".
  "Nimesoma kitu hive karibuni kutoka kwa Sir Alex Ferguson akisema kwamba Van Gaal atahitaji muda na yuko sahihi. Katika mwanzo wake, hata Sir Alex hakushinda chochote ndani ya miaka michache na ulikuwa wakati mgumu kwake kuiunganisha timu kama alivyotaka,"amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO: MAN UNITED MPENI MUDA VAN GAAL AFANYE MAMBO YAWE MAMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top