• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 30, 2014

  HANS POPPE AFIWA NA MAMA MZAZI

  Hans Poppe na mama yake kushoto
  MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amefiwa na mama yake mzazi, Anna Mercati Poppe aliyefariki dunia asubuhi ya leo.
  Mama Poppe amefariki akiwa na umri wa miaka 84, nyumbani kwa mwanawe, Zacharia eneo la Ununio, Mbezi Beach, Dar es Salaam.
  Msiba upo Ununio kwa Hans Poppe na mwili utaagwa Jumamosi saa 4:00 asubuhi kabla ya safari ya kuelekea Iringa kwa mazishi.
  Poppe amesema mazishi yatafanyika katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa, jirani na Chuo Kikuu cha Mkwawa. Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu. Amin.
  Pigo la familia; Bi Anna Mercati Poppe akiwa wanawake enzi zake uhai wake. Kutoka kushoto ni Eddie, mama yao, Zacharia, Sophia, Caesar na Aldo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HANS POPPE AFIWA NA MAMA MZAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top