MAGURI AWAPA RAHA SIMBA SC, APIGA BAO PEKEE MNYAMA AKIUA 1-0 IRINGA
Mshambuliaji Elias Maguri amefunga bao pekee Simba SC ikishinda 1-0 dhidi ya Lipuli ya Iringa katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja Samora mjini Iringa. Simba SC ikiweka kambi Iringa kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi Uwanja Jamhuri mjini Morigoro.
0 comments:
Post a Comment