• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 27, 2014

  YANGA SC WAWEKA KAMBI KAHAMA KUJIANDAA NA MECHI NA KAGERA SUGAR

  Na Prince Akbar, SHINYANGA 
  YANGA SC imetua mjini Kahama, Shinyanga kuweka kambi fupi kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi Kagera Sugar mjini Bukoba Jumamosi.
  Timu hiyo ya kocha Marcio Maximo, itacheza mchezo mmoja wa kirafiki kesho kabla ya kuaza safari ya kuelekea Bukoba kwenye vita ya pointi tatu nyingine za ubingwa wa Bara.
  Jumamosi, Yanga SC ilijiweka sawa kwenye mbio za ubingwa baada ya kuilaza mabao 3-0 Stand United Uwanja wa Kambarage, Shinyanga- Jerry Tegete akifunga mawili kipindi cha pili na Genilson Santana Santos ‘Jaja’ akifunga la kwanza kipindi cha kwanza.
  Kocha Marcio Maximo ameweka kambi Kahama na timu yake kujiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar

  Ushindi huo, umeifanya Yanga SC itimize pointi 10 na kulingana na mabingwa watetezi, Azam FC katika nafasi ya pili, nyuma ya Mtibwa Sugar yenye pointi 13.  
  Wapinzani wao, Kagera Sugar tayari wapo nyumbani Bukoba, ambako Jumamosi walitoa sare ya 1-1 na Coastal Union ya Tanga katika mfululizo wa ligi hiyo.
  Kagera imeweka kambi kijijini kwake, Misenyi wilaya ya Bukoba Vijijini kujiandaa na mchezo huo waliopania kushinda Jumamosi baada ya sare mbili mfululizo nyumbani, nyingine na Stand United wiki iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WAWEKA KAMBI KAHAMA KUJIANDAA NA MECHI NA KAGERA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top