MSHAMBULIAJI Wayne Rooney anajiamini ataweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyeifungia mabao mengi zaidi timu yake ya taifa, England kwa kuvunja rekodi iliyowekwa na Sir Bobby Charlton.
Rooney anashika nafasi ya nne kwa kuifungia mabao mengi England 41, yakiwa matatu nyuma ya Jimmy Greaves, saba nyuma ya Gary Lineker na nane nyuma ya Charlton mwenye mabao 49.
Rooney, ambaye ana umri wa miaka 28 tu, ndiye Nahodha wa kikosi cha timu hiyo kwa sasa ambacho kitamenyana na San Marino Uwanja wa Wembley usiku wa leo. "Ni wakati wangu sasa kuwapiku wote. Najihisi naweza kabisa kufanya hivyo. Hiyo itakuwa heshima kubwa,"amesema.
WAKALI WA MABAO WA KIHISTORIA ENGLAND
Sir Bobby Charlton - Mabao 49 katika mechi 106
Gary Lineker - Mabao 48 katika mechi 80
Jimmy Greaves - Mabnao 44 katika mechi 57
0 comments:
Post a Comment