• HABARI MPYA

    Thursday, October 09, 2014

    INTER MILAN WAMTAKA MTOTO WA PELE, ILA MARSEILLE KUMUACHIA NDIYO SHUGHULI!

    KLABU ya Inter Milan imefufua mango wake wa kutaka kumsajili mwanasoka wa kimataifa wa Ghana, Andre Ayew.
    Vyombo vya Habari Ufaransa vimeripoti kwamba klabu hiyo ya Italia inamfuatilia kwa makini wing huyo wa Ghana, Ayew (pichani chini) ambaye Mkataba wake unamalizika katikati ya mwaka 2015.
    Nia ya ya kumsajili kiungo huyo wa Ghana kutoka klabu hiyo hii si mara ya kwanza, kwani amekuwa akihusishwa na mango wa kuhamia huko tangu mwaka 2011. Ayew hajawahi kuonyesha nia ya kuondoka Marseille.
    Huku Liverpool na Newcastle nazo zikiwa kwenye orodha ya klabu zinazotajwa kumuwania mchezaji huyo pia, Ayew hawezi kuuzwa kwa dau la chini ya Euro Milioni 11.
    Lakini chini ya kocha mpya, Marcelo Bielsa, mtoto huyo wa Abedi Pele ameanza kurudi kwenye kiwango chake na bila shaka itakuwa vigumu kwa klabu yake kumuachia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: INTER MILAN WAMTAKA MTOTO WA PELE, ILA MARSEILLE KUMUACHIA NDIYO SHUGHULI! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top