• HABARI MPYA

    Thursday, October 09, 2014

    ORLANDO PIRATES KUPA MAKALI SIMBA SC IITEKETEZE YANGA OKTOBA 8 TAIFA

    Na Princess Asia, JOHANNESBURG
    SIMBA SC keshokutwa (Jumamosi) itacheza mchezo wa kirafiki na wenyeji Orlando Pirates mjini Johannesburg, Afrika Kusini katika sehemu ya maandalizi yake ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, Oktoba 18, mwaka huu Dar e Salaam.
    Katika mchezo huo, Simba SC itawakosa wachezaji wake walio timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Uganda, The Cranes- ambao wanatarajiwa kujiunga na wenao kuanzia Jumatatu.
    Hata hivyo, mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga na The Cranes yeye hatakwenda kabisa Afrika Kusini, kwa sababu timu yake hiyo ya taifa itakuwa na mechi ya kufuzu AFCON katikati ya wiki. 
    Kocha Patrick katikati na wachezaji wake baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa O. Tambo Afrika Kusini usiku wa jana

    Wachezaji wa Simba SC walioko Stars ni; mabeki Miraji Adam na Joram Mgeveke na viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo ambao wote watakwenda Afrika Kusini Jumatatu.
    Simba SC imefikia katika hoteli ya Eden Vale Petra na itakuwa inafanya mazoezi kwenye viwanja wa Eden Vale mjini Johannesburg. 
    Msafara wa kwanza Simba SC uliondoka jioni ya jana kwa ndege ya Fast Jet ukiongozwa na kocha Mkuu, Mzambia Patrick Phiri- wakati kocha wa makipa, Iddi Pazi ‘Father’ ameachwa Dar es Salaam.
    Simba SC itakuwa ikifanya mazoezi ya nguvu hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya mechi na watani.
    Baada ya sare tatu mfululizo katika mechi zake tatu za awali, 2-2 na Coastal Union, 1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand United, Simba SC imepania kushinda mechi ya kwanza Oktoba 18.  
    Wachezaji wa Simba SC wakiwa kwenye baso dogo kuelekea hotelini baada ya kuwasili Johannesburg usiku wa jana
    Wachezaji wa Simba SC wakipata chakula katika hoteli ya Eden Vale
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ORLANDO PIRATES KUPA MAKALI SIMBA SC IITEKETEZE YANGA OKTOBA 8 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top