• HABARI MPYA

    Friday, October 10, 2014

    NOOIJ ASEMA ATAPANGA WAREFU STARS NA BENIN

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij amesema katika mchezo wa keshokutwa wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin atatoa kipaumbele kwa wachezaji warefu kwenye kikosi chake.
    Kocha huyo wa zamani wa Ethiopia na Msumbiji ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba atafanya hivyo kwa sababu wapinzani wao, Benin kikosi chao kinaundwa na wachezaji warefu zaidi.

    Kocha Mart Nooij amesema atawapa kipaumbele wachezaji warefu kwenye mechi na Benin Jumapili

    REKODI YA MART NOOIJ TAIFA STARS 

    Tanzania 0-0 Malawi (Kirafiki Mbeya)
    Tanzania 1-0 Zimbabwe (Kufuzu AFCON Dar es Salaam)
    Tanzania 1-0 Malawi (Kirafiki Taifa)
    Tanzania 2-2 Zimbabwe (Kufuzu AFCON Harare)
    Tanzania 2-4 Botswana (Kirafiki Gaborone)
    Tanzania 2-2 Msumbiji (Kufuzu AFCON Dar es Salaam)
    Tanzania 1-2 Msumbiji (Kufuzu AFCON Maputo)
    Burundi 
    Tanzania 0-2 Burundi (Kirafiki Bujumbura)
    Nooij amesema kwamba lengo lake ni kuona kunakuwa na mapambano sawa katika kuwania mipira ya juu. “Itakuwa tofauti na kupanga wachezaji wafupi wengi, ambao wanaweza kuwapa wepesi Benin katika kushinda mipira mingi ya juu,”amesema.
    Aidha, Nooij amesema katika mchezo huo atatumia mabeki watatu wa kati, ili kuwa na ukuta mgumu, mmoja wao akicheza kama kiungo mkabaji ili kuwapunguzia wenzake majukumu.
    Amesema mpango huo unakuja kufuatia makosa yaliyofanywa na timu yake katika mechi ya mwisho dhidi ya Burundi ambayo ndani ya dakika 15 za kwanza walijikuta wanafungwa mabao mawili ya haraka haraka dakika ya kwanza na 12.
    Kwa ujumla, tangu ametua Stars Nooij ameiongoza Stars katika mechi nane na kati ya hizo, ameshinda mbili amefungwa tatu na kutoa sare tatu na katika mechi zote hizo nyavu za Stars zimetikiswa mara 12, huku yenyewe ikifunga mabao tisa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NOOIJ ASEMA ATAPANGA WAREFU STARS NA BENIN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top