• HABARI MPYA

    Friday, October 10, 2014

    PIRES AMVAA WENGER NA KUMUAMBIA; "KAMA UNATAKA UBINGWA, NUNUA SAMI KHEDRIA, NI VIEIRA MPYA"

    KLABU ya Arsenal imeshauriwa kumsajili nyota wa Real Madrid, Sami Khedira ifikapo Januari kama wanataka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu, kwa mujibu wa kiungo wa zamani wa Washika Bunduki hao, Robert Pires.
    Pires anafahamu mini kinahitajika ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England, kwani alitwaa mataji hayo mara mbili akiwa na The Gunners.
    Na Mfaransa huyo ambaye amesaini Goa FC katika Ligi Kuu mpya ya India anaamini kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anahitaji kiungo mchezeshaji.

    Sami Khedira aliisaidia Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia mwaka huu

    Pires ameliambia gazeti la The Daily Telegraph: "Yeye [Wenger] anahitaji mchezaji mkubwa katika kiungo, kama (Patrick) Vieira, mwenye nguvu, mrefu, kwa sababu nafasi hii ni muhimu sana kujenga uwiano baina yasafu ya ushambuliaji na ulinzi.
    "Ubora huo upo pale, lakini unahitaji zaidi, labda  [mtu kama] Yaya Toure. Ananikumbusha mimi enzi za Patrick Vieira, labda wana nafasi kwa Khedira.
    "Ni kama kwenye dirisha la usajili la Januari. Anaichezea vizuri sana Ujerumani. Ushauri wangu ni kama ikiwa anaweza kumnunua Khedira anaweza kuwa [new] Vieira, mpiganaji zaidi kwenye kiungo," amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIRES AMVAA WENGER NA KUMUAMBIA; "KAMA UNATAKA UBINGWA, NUNUA SAMI KHEDRIA, NI VIEIRA MPYA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top