• HABARI MPYA

    Friday, October 10, 2014

    WAZIRI ATEUA WAJUMBE WATATU WAPYA BARAZA LA MICHEZO

    Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
    WAZIRI wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar, Said Ali Mbarouk (pichani chini) amewateua Wajumbe watatu wapya wa Baraza la Taifa la Michezo la Zanzibar (BMZ).
    Wajumbe hao ni Ndugu Ameir Mohamed Makame kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
    Wengine ni Hassan Kificho kutoka Idara ya Watu wenye Ulemavu na Khamis Abdallah Said kutoka Wadau wa Michezo.
    Taarifa ya Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar imesema kwamba uteuzi huo unaanza leo Oktoba 10, 2014.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI ATEUA WAJUMBE WATATU WAPYA BARAZA LA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top