• HABARI MPYA

    Monday, October 06, 2014

    KINDA AZAM AONGEZWA STARS, NOOIJ SASA ANA WAKALI 10 WA CHAMAZI KIKOSI CHA KUIVAA BENIN

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa Tanzania Bara, Azam FC sasa watakuwa na wachezaji 10 katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichoingia kambini leo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin Oktoba 12, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hiyo inafuatia kocha Mholanzi, Mart Nooij kumuongeza kikosini beki wa kushoto wa timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake, Gardiel Michael leo. 
    Kinda huyo aliyepandishwa msimu huu kutoka akademi ya klabu hiyo, anakwenda kuungana na makipa Aishi Manula na Mwadini Ali, mabeki Said Moradi, Shomari Kapombe na Aggrey Morris, viungo Erasto Nyoni, Himid Mao na Salum Abubakar na mshambuliaji Khamis Mcha ‘Vialli’.
    Gardiel Michael kulia ameongezwa Taifa Stars

    Hiyo ni idadi kubwa zaidi miongoni mwa klabu zilizozotoa wachezaji wa kikosi cha Mholanzi Mart Nooij kwa ajili ya mechi hiyo ya Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na kama si kuwa majeruhi, mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’ angefanya idadi ya wachezaji 11 wa Azam Taifa Stars.
    Kikosi kamili Stars ni; Makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).
    Mabeki ni Gardiel Michael (Azam FC), Said Mourad (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
    Viungo ni Jonas Mkude (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).
    Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KINDA AZAM AONGEZWA STARS, NOOIJ SASA ANA WAKALI 10 WA CHAMAZI KIKOSI CHA KUIVAA BENIN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top