• HABARI MPYA

    Monday, October 06, 2014

    AIRTEL YAZINDUA SHINDANO LA KUIBUA VIPAJI VYA MUZIKI KUPITIA SIMU YA MKONONI

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mashindano ya kusaka vipaji vya muziki kupitia simu ya mkononi yajulikanayo kama Airtel TRACE Music Star kwa lengo la kukuza vipaji vya muziki na kuwawezesha wanamuziki chipukizi wa kitanzania kujulikana katika anga
    za muziki duniani.
    Uzinduzi huu umefatia ushirikiano kati ya Airtel na Kampuni Muziki ya TRACE pamoja na mwanamuziki nguli wa Marekani, Akon. 
    Mashindano haya mbali na kufanyika nchini Tanzania pia yatashirikisha vijana kutoka nchi 13 barani Afrika ambazo Airtel inafanya biashara zake, nchi hizo ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, The Democratic
    Republic of Congo (DRC), na Gabon, ambapo waimbaji bora kutoka kwenye kila nchi watachaguliwa na kuzawadiwa baada ya kuingizwa kwenye mashindano ya waimbaji bora kutoka nchi nyingine ili kupata mshindi atakayetwaa taji la Mwanamuziki mwenye kipaji bora Afrika. 
    Mwanamuziki Ommy Dimpoz akitumbuiza kwenye shughuli hiyo


    Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiwa na msaani wa muziki wa kizazi kipya Lady JD wakati wa uzinduzi wa Airtel Trace Music Star

    Mshindi wa Afrika atajishindia zawadi mbalimbali ikiwemo
    kurekodi na kusambaziwa nyimbo zake chini ya studio kubwa ulimwenguni pamoja na kufaidika na mafunzo ya kufuliwa kimuziki na Nguli wa Muziki wa Amerika Akon
    Akiongea wakati wa uzinduzi wa program hiyo Mkurugenzi wa Masoko bwana Levi Nyakundi alisema” mpango huu unaenda sambamba na dhamira yetu wa kuwawezesha vijana wenye ndoto ya kuwa wanamuziki bora kuonyesha uwezo wao kuwawezesha kufikia ndoto zao. 
    Tunafahamu kuwa Tanzania ina vijana wengi wenye vipaji vya muziki lakini bado hawajajulikana katika anga za muziki na ndio maana leo tunazindua program hii na kuwawezesha
    kujiunga kirahisi kupitia simu yake ya mkononi na kushirikisha Airtel Trace Music Stars na kuibuka kuwa wanamziki bora”
    Mashindano haya yatakayoenda kwa muda wa mienzi sita yanaanza kuanzia rasmi hapa nchini siku octoba 7 2014 ambapo mshiriki yeyote atakayependa kushiriki atatakiwa kupiga 0901002233, na kuimba nyimbo zake kwa kutumia simu yake na kutuma kwenye namba hii, kisha nyimbo
    zake zitasikilizwa na kuchagulia kufudhu kuingia kwenye kinyanganyiro na kuweza kupigiwa kura kuibuka kuwa mwimbaji nyota wa Tanzania na baadae kuwa super star wa Afrika kwa ujumla.
    Halikadhalika mashabiki na wapenzi wa muziki wataweza kumpigia kura mshiriki wanayempenda ili kumuwezeshwa nyimbo zake kushinda, ili kumpigia kura mshiriki wako tuma namba/code ambayo mshiriki ataitangaza pindi nyimbo yake itakapochaguliwa kuingia kwenye mashindano au unaweza kuipata wewe mwenyewe kwenye tovuti www.tracemusicstar.com’’Aliongeza Nyakundi.
    Akiongea kuhusu program hiyo Mwanamuziki wa Bongo Flava Ommy Dimples alisema’ kwa hakika haya ni mashindano ya pekee yanayotoa fulsa kwa mwanamziki yeyote ambaye angependa kuwa superstar kushiriki.
    Napenda kuwahamasisha vijana kuchangamkia fulsa hii kwa kurekodi freestyle yako ya flave yoyote kali kupitia simu yako na kutuma nyimbo yako. Pia napenda kuwaomba mashabiki na wapenzi wa muziki kuwapigia kura washiriki hawa kwa wingi ili kuweza kumpata ushindi.
    kwa wanamuziki chipukizi mashindano haya si yakukosa maana wewe pia unaweza kuibuka kuwa superstar wa Airtel Trace Music Star kwa njia rahisi tu Piga, Imba, Shinda. aliongeza Dimples Airtel imeingia mkataba wa ushirikiano na Trace Music kwa muda wa miaka mitatu ambapo Fainali ya mashindano haya ya Airtel Trace Music 2014 yanategemea kufanyika Mwezi March 2015.
    Zawadi nyingine zitakazotoliwa kwa washindi wa mashindano haya ni pamoja na pesa taslimu na simu za mkononi Kwa maelezo zaid tembelea tovuti ya: www.tracemusicstar.com/ Facebook: https://www.facebook.com/airteltracemusicstar
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AIRTEL YAZINDUA SHINDANO LA KUIBUA VIPAJI VYA MUZIKI KUPITIA SIMU YA MKONONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top