• HABARI MPYA

    Monday, October 06, 2014

    FUNDI MKUDE AONGEZWA STARS YA KUKIPIGA NA BENIN

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij amemuongeza kiungo wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude katika kikosi kitakachomenyana na Benin mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Oktoba 12 mwaka huu mjini Dar es Salaam.
    Mkude alikuwa majeruhi baada ya kuumia akiichezea Taifa Stars mchezo wa kirafiki na Botswana mjini Gaborone Juni mwaka huu na ana wiki mbili sasa tangu amerudi uwanjani.
    Baada ya kucheza vizuri mechi mbili mfululizo, dhidi ya Polisi Moro na Stand United, zote Simba SC ikitoa sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa, Mkude anarejeshwa Stars na anaingia kambini leo.
    Kiungo Jonas Mkude ameongezwa Taifa Stars itakayomenyana na Benin

    Wachezaji wengine waalioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).
    Mabeki ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
    Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).
    Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FUNDI MKUDE AONGEZWA STARS YA KUKIPIGA NA BENIN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top