MCHEZAJI wa zamani wa Coastal Union ya Tanga, Ahmed Seif amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake, Usagara, Tanga akiwa na umri wa miaka 70 na ushei.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa marehemu na mchezaji mwenzake wa zamani hadi timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, John Lyimo, Ahmed Seif alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya sukari.
Lyimo amesema msiba upo barabara ya tisa ambako ni nyumbani kwao marehemu na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho Saa 4:00 asubuhi.
Enzi za uhai wake miaka ya 1970, marehemu Seif aliyekuwa anacheza nafasi za kiungo na ushambuliaji, alikuwa anasifika kwa kupiga mashuti makali.
Kiungo wa zamani wa Simba SC, Khalid Abeid aliyecheza naye marehemu timu ya taifa, amemuelezea kwamba alikuwa mchezaji hodari na mtu mwema.

![]() |
Mashabiki wa Coastal wamepata msiba, mchezaji wao wa zamani amefariki dunia |
Lyimo amesema msiba upo barabara ya tisa ambako ni nyumbani kwao marehemu na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho Saa 4:00 asubuhi.
Enzi za uhai wake miaka ya 1970, marehemu Seif aliyekuwa anacheza nafasi za kiungo na ushambuliaji, alikuwa anasifika kwa kupiga mashuti makali.
Kiungo wa zamani wa Simba SC, Khalid Abeid aliyecheza naye marehemu timu ya taifa, amemuelezea kwamba alikuwa mchezaji hodari na mtu mwema.
0 comments:
Post a Comment