• HABARI MPYA

    Saturday, February 01, 2014

    BERBATOV ATUA MONACO KUZIBA PENGO LA FALCAO

    MSHAMBULIAJI Dimitar Berbatov amejiunga na Monaco ya Ufaransa kwa mkopo kutoka Fulham hadi mwishoni mwa msimu.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33amechagua kuhamia Ligue 1 badala ya kurejea Tottenham iliyomtaka pia.
    Hakuna kurudi: Dimitar Berbatov ameondoka Fulham na kutua Monaco ingawa Spurs walimtaka pia

    Vimwaga fedha Monaco wamemchukua Berbatov azibe pengo la mshambuliaji wao nyota Radamel Falcao, ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti wiki iliyopita.
    Kocha Rene Meulensteen alikuwa akikimbizana ile mbaya kupata saini ya mchezaji huyo katika siku ya leo ya mwisho ya usajili wa dirisha dogo Ulaya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BERBATOV ATUA MONACO KUZIBA PENGO LA FALCAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top