• HABARI MPYA

  Thursday, November 16, 2017

  AZAM FC KUMKOSA MAO NA MABEKI WOTE WAWILI WA GHANA DHIDI YA NJOMBE

  Na Mwandishi Wetu, NJOMBE
  AZAM FC itamkosa Nahodha wake, Himid Mao katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Njombe Mji FC Jumapili Uwanja wa Saba Saba, kwa sababu anatumikia adahbu ya kadi tatu za njano. 
  Pamoja na kiungo wake huyo mahiri, Azam pia itawakosa mabeki Waghana Daniel Amoah na Yakubu Mohammed ambao nao pia wamefikisha kadi tatu za njano.
  Kikosi cha Azam kipo Njombe tangu Saa 1 usiku wa jana kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi Kuu baada ya safari ndefu ya saa 15 barabarani  baada ya kuondoka Dar es Salaam Saa 10 Alfajiri.
  Awali, mchezo huo ilikuwa ufanyike Jumamosi lakini ukasogezwa mbele kwa maombi ya wamiliki haki za matangazo ya Televisheni, Azam TV.
  Himid Mao hatacheza dhidi ya Njombe Mji FC Jumapili Uwanja wa Saba Saba kutokana na kadi tatu za njano

  Wachezaji waliowasili na Azam mjini humo ni makipa Razak Abalora, Mwadini Ally na Benedict Haule, mabeki ni Nahodha Msaidizi Aggrey Morris, David Mwantika, Abdallah Kheri, Bruce Kangwa, Hamim Karim na Swaleh Abdallah.
  Viungo ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo ‘Chumvi’, Salmin Hoza, Stephan Kingue, Enock Atta Agyei, Ramadhani Singano ‘Messi’, Joseph Mahundi, Idd Kipagwile na washambuliaji ni Mbaraka Yusuph, Waziri Junior, Yahya Zayd na Andrea Simchimba, aliyepandishwa wiki iliyopita kutoka timu ya vijana.
  Katika mechi tisa ambazo Azam FC imecheza hadi sasa, imeshinda tano na kutoka sare nne hivyo kujikusanyia pointi 19 sawa na Simba inayoongoza Ligi Kuu kwa wastani wa mabao.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC KUMKOSA MAO NA MABEKI WOTE WAWILI WA GHANA DHIDI YA NJOMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top