• HABARI MPYA

  Saturday, January 09, 2016

  MFALME WA AFRIKA, SAMATTA APATA MAPOKEZI MAZURI AKIWASILI NA TUZO YAKE

  Waandishi maarufu wa habari za michezo Tanzania, Tullo Chambo (kushoto) na Salum Mkandemba (kulia) wa gazeti la Tanzania Daima wakiwa na Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, Mbwana Ally Samatta (katikati) baada ya kuwasili Alfajiri ya leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kufatia kushinda tuzo hiyo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) usiku wa juzi mjini Abuja, Nigeria 
  Wapenzi na mashabiki maarufu wa soka nchini, Esther na Bob Chicharito (kulia) walijitokeza pia kumlaki Samatta. Mshambuliaji huyo wa TP Mazembe ya DRC alipata mapokezi mazuri licha ya kuwasili usiku wa manane
  Wapenzi mbalimbali wa soka wakimkabidhi zawadi Mbwana Samatta Uwanja wa Ndege wa JNIA
  Kutoka kulia ni Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo, Samatta mwenyewe na mchezaji mwenzake wa Tanzania na TP Mazembe, Thomas Ulimwengu
  Mwandishi maarufu wa habari za michezo, Mwani Nyangassa naye alijitokeza akiwa na fulana maalum ya "Hongera Samatta'

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MFALME WA AFRIKA, SAMATTA APATA MAPOKEZI MAZURI AKIWASILI NA TUZO YAKE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top