• HABARI MPYA

    Wednesday, January 06, 2016

    KLOPP ASEMA LIVERPOOL LAZIMA ISAJILI BEKI DIRISHA DOGO

    Jurgen Klopp amesema Liverpool inalazimika kusajili beki dirisha dogo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    ORODHA YA MAJERUHI HIVI SASA LIVERPOOL

    Philippe Coutinho - Nyama
    Dejan Lovren - Nyama
    Divock Origi - Nyama
    Daniel Sturridge - Nyama
    Martin Skrtel - Nyama
    Jordan Rossiter - Nyama 
    Mamadou Sakho - Majeruhi 
    Jordan Henderson - Majeruhi
    Joe Gomez - Goti
    Danny Ings - Goti 
    KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp klabu italazimika kusajili beki katika dorisha dogo kutokana na kuandamwa na baa la majeruhi.
    Philippe Coutinho na Dejan Lovren wote wameumia nyama timu ikishinda 1-0 dhidi ya Stoke katika mchezo wa kwanza Nusu Fainali ya Kombe la Ligi. 
    Martin Skrtel tayari yuko nje ya Uwanja kutokana na maumivu ya nyama na naye anasumbuliwa na maumivu ya mguu, Mamadou Sakho anasumbuliwa na goti na Kolo Toure aliumia Uwanja wa Britannia Stadium, maana yake Klopp anakabiliwa na tatizo la mabeki wa kati.
    Liverpool inataka kumsajili beki wa Schalke, Joel Matip lakini mpango wowote wa kumsajili beki huyo wa kimataifa wa Cameroon, hauwezi kufanikiwa hadi mwishoni mwa msimu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KLOPP ASEMA LIVERPOOL LAZIMA ISAJILI BEKI DIRISHA DOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top