• HABARI MPYA

  Sunday, January 10, 2016

  FARID MUSSA 'AWA LULU' AZAM FC, DILI LA SLOVENIA LAPIGWA CHINI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imesitisha mpango wa kumpeleka winga wake, Farid Mussa Malik Hispania kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa baada ya kupata ofa nyingine nzuri juu ya kinda huyo wa kimataifa wa Tanzania.
  Farid alitarajiwa kuondoka wiki hii kwenda Hispania kuungana na klabu bingwa ya Slovenia, FC Olimpija Ljubljana iliyoweka kambi huko ambako amepewa siku 10 za majaribio.
  Mabingwa hao wa Slovenia wameweka kambi nchini Hispania kujiandaa na Ligi ya kwao na Farid alitarajiwa kuwa nao kwa siku zote 10 akifanya nao mazoezi kabla ya kuamua kumununua. 
  Farid Mussa (kulia) akiwatoka mabeki wa Yanga SC katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya Bara
  Hata hivyo, kufuatia kutokea wakala mwingine ambaye amewaahidi Azam FC kumpatia Farid timu kubwa zaidi na maslahi mazuri, mpango wa kwenda Hispania ukafutwa na winga huyo akaenda kujiunga na kikosi cha timu yake katika Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar. 
  Baada ya Azam FC kutolewa hatua ya makundi tu ya michuano hiyo, Farid amerejea na kikosi cha timu yake Dar es Salaam kuendelea na maandalizi ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FARID MUSSA 'AWA LULU' AZAM FC, DILI LA SLOVENIA LAPIGWA CHINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top