• HABARI MPYA

  Monday, January 18, 2016

  CAMEROON WAWATANDIKA 1-0 ANGOLA CHAN 2016, LEO NI NIGERIA NA NIGER

  TIMU ya taifa ya Cameroon jana imeanza vyema Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika, baada ya kuifunga bao 1-0 Angola 1-0 katika mchezo wa Kundi licha ya kucheza pungufu ya mchezaji mmoja Uwanja wa Huye, Kigali, Rwanda.
  Ushindi huo wa Simba Wasiofungika unawafanya walingane kwa pointi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao walishinda 3-0 dhidi ya Ethiopia 3-0 mapema jana katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo.
  Bao pekee la Cameroon jana lilifungwa na mshambuliaji wa Coton Sport de Garoua, Yazid Atouba kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 23.

  Mshambuliaji wa Cameroon, Yazid Atouba (kulia) akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Angola jana

  Cameroon ililazimika kucheza kwa kujihami zaidi kulinda ushindi wake, baada ya beki Joseph Ngwem kutolewa kwa kadi nyekundu dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika.
  Cameroon itashuka tena dimbani Jumatano kumenyana na Ethiopia wakati Angola itaivaa DRC mjini Huye.
  Michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, inaendelea kwa mechi za Kundi C, Tunisia ikimenyana na Guinea na Nigeria ikivaana na maajirani, Niger.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON WAWATANDIKA 1-0 ANGOLA CHAN 2016, LEO NI NIGERIA NA NIGER Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top