• HABARI MPYA

  Thursday, July 06, 2023

  YANGA YAAMBULIA SARE KWA BIG BULLETS MALAWI LEO


  TIMU ya Yanga imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Nyasa Big Bullets leo Uwanja wa Bingu Mutharika Jijini Lilongwe nchini Malawi.
  Mchezo huo wa kuazimisha miaka 59 ya Uhuru wa Malawi ulihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake, Dk. Lazarus McCarthy Chakwera Rais wa nchi hiyo ambao walitazama mchezo kwa kipindi cha kwanza pekee.
  Yanga ilipata pigo katika mchezo huo baada ya winga wake chipukizi, Dennis Nkane kuumia dakika ya 21 na kushindwa kuendelea na mchezo hivyo kukimbizwa hospitali kwa gari maalum la wagonjwa, Ambulance.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAAMBULIA SARE KWA BIG BULLETS MALAWI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top