• HABARI MPYA

  Thursday, July 06, 2023

  MKENYA NDIYE MENEJA MPYA WA SIMBA SC


  KLABU ya Simba imemtambulisha Mkenya, Mikael Igendia kuwa Meneja wake mpya wa timu na Mkuu wa Sayansi ya Michezo kwa mkataba wa miaka miwili.
  Igendia (36) anachukua nafasi ya Patrick Rweyemamu ambaye amekuwa Mkuu wa Programu za soka la vijana.
  Igendia amewahi kufanya kazi na Gormahia FC, timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
  Uwepo wa Igendia kwenye kikosi ni sehemu ya kuliboresha benchi lake la ufundi kuelekea msimu mpya wa Ligi 2023/24.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKENYA NDIYE MENEJA MPYA WA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top