WINGA wa Yanga SC, Dennis Nkane aliyeumia na kukimbizwa hospitali leo wakati wa mchezo wa kirafiki na wenyeji, Nyasa Big Bullets Uwanja wa Bingu Mutharika Jijini Lilongwe nchini Malawi anaendelea vizuri.
Katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bila mabao, Nkane aliumia dakika ya 21 na kushindwa kuendelea hivyo kukimbizwa hospitali kwa gari maalum la wagonjwa, Ambulance.
Lakini tayari Nkane amekwishafanyiwa matibabu na kurejea kambini kuungana na wenzake kwa ajili y safari ya kurejea nyumbani.
Mchezo huo wa kuazimisha miaka 59 ya Uhuru wa Malawi ulihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake, Dk. Lazarus McCarthy Chakwera Rais wa nchi hiyo ambao walitazama kipindi cha kwanza pekee.
0 comments:
Post a Comment