MSHAMBULIAJI mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Ilunga Mbombo amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuchezea Azam FC hadi mwaka 2024.
Idris Mbombo aliyejiunga na Azam FC mwaka 2021 akitokea Gouna FC ya Misri amekuwa tegemeo la upachikaji mabao Azam FC ambaye kwenye misimu miwili iliyopita ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara amefunga jumla ya mabao 17.
0 comments:
Post a Comment