• HABARI MPYA

  Friday, July 07, 2023

  CAF YABADILI MFUMO MICHUANO YA KLABU AFRIKA


  SHIRIKISHO la Soka Afrika limeamua kuyatenganisha mashindano yake ya ngazi ya klabu na kuanzia msimu ujao hakuna timu itakayodondokea kwenye Kombe la Shirikisho kutoka Ligi ya Mabingwa.
  Kamati ya Utendaji ya CAF katika kikao chake cha leo mjini Rabat nchini Morocco imeamua hakutakuwa na mechi za Raundi ya Pili ya nyongeza ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.
  Timu 16 zitakazofuzu Raundi ya Pili ya mchujo zitakwenda moja kwa moja Hatua ya makundi kote, kwenye Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho na zitakazotolewa safari yao itaishia hapo.
  Kwa msimu ujao, 2023-2024 Tanzania itawakilishwa na Yanga na Simba katika Ligi ya Mabingwa na Azam FC na Singida Fountain Gate katika Kombe la Shirikisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YABADILI MFUMO MICHUANO YA KLABU AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top