• HABARI MPYA

  Tuesday, May 02, 2023

  TFF YAAHIRISHA MECHI YA YANGA NA SINGIDA KOMBE LA TFF


  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeuahirisha mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya wenyeji Singida Big Stars na mabingwa watetezi, Yanga uliopangwa kufanyika Jumapili ya Uwanja wa LITI, Singida.
  Hiyo inafuatia ombi la klabu ya Yanga kwa TFF ili wapate muda kidogo wa kujiandaa na mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants Mei 10 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Sasa Yanga itamenyana na Singida Big Stars Alhamisi tu katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kabla ya kurejea Dar es Salaam kuisubiri Marumo Gallants.
  Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu, Yanga imebakiza jumla mechi nne za Ligi Kuu pamoja na huo wa Singida Big Stars, nyingine dhidi ya Dodoma Jiji, Mbeya City na Tanzania Prisons zote ugenini na wanatakiwa kushinda mechi tatu ili kuwa mabingwa tena.
  Mechi ya marudiano na Marumo Gallants itafanyika Afrika Kusini Mei 17.
  Wakati huo huo mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza ya ASFC baina ya Azam FC na Simba uliopangwa kufanyika Jumamosi Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara umesogezwa mbele kwa siku moja hadi Jumapili.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAAHIRISHA MECHI YA YANGA NA SINGIDA KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top