// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA IMEANDIKA HISTORIA JALILI, ASEMA RAIS DK. SAMIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA IMEANDIKA HISTORIA JALILI, ASEMA RAIS DK. SAMIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, May 02, 2023

  YANGA IMEANDIKA HISTORIA JALILI, ASEMA RAIS DK. SAMIA


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kusema imeandika historia Jalili.
  “Pongezi kwa Klabu ya Yanga kwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup), na kila la kheri katika maandalizi mliyoanza sasa kwa mchezo ujao. Mmeandika historia jalili,”amesema Rais Samia na kuongoza;
  “Mmetuheshimisha sana. Hamasa yangu inaendelea, na sasa imeongezeka. Kaifanyeni kazi,”.
  Yanga SC ilitinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili licha ya sare ya bila kufungana na Rivers United ya Nigeria katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Yanga imekwenda Nusu Fainali kwa faida ya ushindi wa 2-0 ugenini kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyotangulia nchini Nigeria, mabao ya mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele kipindi cha pili.
  Yanga sasa itamenyana na Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambayo imeitoa Pyramids ya Misri kwa jumla ya mabao 2-1, ikitoa sare ya 1-1 Cairo wiki iliyopita na kushinda 1-0 leo Phokeng, NW.
  Mechi ya kwanza Yanga na Marumo Gallants itafanyika Dar es Salaam Mei 10 na marudiano yatafuatia Afrika Kusini Mei 17.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA IMEANDIKA HISTORIA JALILI, ASEMA RAIS DK. SAMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top