• HABARI MPYA

  Thursday, May 04, 2023

  SALAH AFUNGA BAO PEKEE LIVERPOOL YASHINDA 1-0


  BAO la Nyota Mmisri, Mohamed Salah dakika ya 39 kwa penalti limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumatano Uwanja wa Anfield.
  Penalti hiyo ilitolewa baada ya Darwin Nunez kuangushwa kwenye boksi na Issa Dip na kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 59 katika mchezo wa 34, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi nne na Manchester United ambayo pia ina mechi mbili mkononi.
  Kwa upande wao Fulham baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 45 za mechi 34 pia nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH AFUNGA BAO PEKEE LIVERPOOL YASHINDA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top