• HABARI MPYA

  Thursday, May 04, 2023

  HAALAND AWEKA REKODI MPYA MAN CITY IKISHINDA 3-0


  MABINGWA watetezi. Manchester City wamerejea kileleni mwa Ligi ya England baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Ham United usiku wa Jumatano Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Nathan Ake dakika ya 50, Erling Haaland dakika ya 70 ambalo linakuwa la 35 linaloweka rekodi msimu huu wa Ligi Kuu na Phil Foden dakika ya 85.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 79 katika mchezo wa 33 na kurejea kileleni ikiizidi pointi moja Arsenal ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.
  Kwa upande wao, West Ham United baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 34 za mechi 34 nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND AWEKA REKODI MPYA MAN CITY IKISHINDA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top