• HABARI MPYA

  Wednesday, May 03, 2023

  SIMBA SC NA NAMUNGO NGOMA DROO, 1-1 RUANGWA


  WENYEJI, Namungo FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Simba SC ilitangulia kwa bao la mshambuliaji wake Mkongo, Jean Othos Baleke dakika ya 27 akimalizia pasi ya kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza.
  Namungo FC wakafanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 38, mfungaji kiungo Hassan Salum Kabunda aliyemalizia mpira uliotemwa na kipa Ally Salum kufuatia kona ya Shiza Kichuya.
  Simba SC inafikisha pointi 64 katika mechi ya 27, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Namungo FC kwa upande wao wanafikisha pointi 36, ingawa wanabaki nafasi ya sita wakizidiwa pointi moja na Geita Gold baada ya wote kucheza mechi 27.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA NAMUNGO NGOMA DROO, 1-1 RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top