• HABARI MPYA

  Friday, May 05, 2023

  BRIGHTON YAICHAPA MANCHESTER UNITED 1-0 THE AMEX


  WENYEJI, Brighton & Hove Albion wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Alhamisi Uwanja wa The Amex na kulipa kisasi cha kutolewa kwenye Kombe la FA.
  Bao pekee la Brighton limefungwa na Alexis Mac Allister dakika ya tisa ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo kwa mkwaju wa penalti kufuatia beki wa Manchester United, Luke Shaw kuushika mpira kizembe kwenye boksi.
  Kwa ushindi huo, Brighton wanafikisha pointi 55 katika mchezo wa 32 na kusogea nafasi ya sita, wakati Manchester United wanabaki na pointi zao 63 za mechi 33 nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRIGHTON YAICHAPA MANCHESTER UNITED 1-0 THE AMEX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top