• HABARI MPYA

  Wednesday, May 03, 2023

  ARSENAL YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND


  WENYEJI, Arsenal wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea usiku huu Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa Martin Odegaard mawili, dakika ya 18 na 31 na Gabriel Jesus dakika ya 34, wakati la Chelsea limefungwa na Chukwunonso Madueke dakika ya 65.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 78 katika mchezo wa 34, ikiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi, Manchester City ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.
  Kwa upande wao Chelsea ambao wanapoteza mechi ya sita mfululizo chini ya kocha wa muda, Frank Lampard wanabaki na pointi zao 39 za mechi 33 nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top