• HABARI MPYA

  Thursday, March 02, 2023

  SIMBA SC YASHINDA 4-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI ASFC


  WENYEJI, Simba SC wamefanikiwa kwenda Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Africans Sports ya Tanga leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Jean Baleke dakika ya 36, beki Kennedy Juma dakika ya 47, mshambuliaji Mzanzibari Mohamed Mussa dakika ya 69 na beki Jimmyson Mwanuke dakika ya 90.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASHINDA 4-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top