• HABARI MPYA

  Wednesday, March 15, 2023

  NI YANGA NA GEITA GOLD, SIMBA NA IHEFU ROBO FAINALI ASFC


  MABINGWA watetezi, Yanga SC watamenyana na Geita Gold katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Jijini Dar es Salaam.
  Watani wao wa jadi,  Simba SC watamenyana na Ihefu SC ya Mbeya Jijini Dar es Salaam pia, wakati Singida Big Stars watakuwa wenyeji wa Mbeya City na Azam FC watawakaribisha Mtibwa Sugar.
  Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi huu na Nusu Fainali zitafuatia mwezi ujao katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na LITI mjini Singida, wakati Fainali itapigwa Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  MECHI ZA ROBO FAINALI ASFC:
  Simba SC vs Ihefu SC
  Singida Big Stars vs Mbeya City
  Yanga SC vs Geita Gold FC
  Azam FC vs Mtibwa Sugar
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI YANGA NA GEITA GOLD, SIMBA NA IHEFU ROBO FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top