MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na Nahodha, beki Bakari Mwamnyeto dakika ya 52, mshambuliaji chipukizi Clement Mzize mawili, dakika ya 70 na 88 kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki kwa penalti dakika ya 85, wakati la Prisons limefungwa na Jumanne Elfadhil dakika ya 60.
Clement Mzize angeweza kuondoka na mpira kama angefunga na mkwaju wa penalti dakika ya dakika za lala salama.
0 comments:
Post a Comment