• HABARI MPYA

  Thursday, March 02, 2023

  MAN UNITED YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA FA


  WENYEJI, Manchester United wametoka nyuma na kushinda 3-1 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Kombe la FA England jana Uwanja wa Old Trafford.
  West Ham ilitangulia na bao la Said Benrahma dakika ya 54, kabla ya United kuzinduka kwa mabao ya  Alejandro Garnacho dakika ya 77, Fred dakika ya 90 na Nayef Aguerd aliyejifunga dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Man United itakutana na Fulham katika Robo Fainali, wakati mahasimu wao, Manchester City watamenyana na Burnley, Brighton na Grimsby ya League Two na Sheffield United dhidi ya Blackburn Rovers, zote za Championship.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top