• HABARI MPYA

  Thursday, March 02, 2023

  ARSENAL ‘IS ON FIRE’, EVERTON YAFA 4-0 EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal wametanua uongozi wao kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Everton jana Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yalifungwa na Bukayo Saka dakika ya 40, Gabriel Martinelli mawili, dakika ya 45 na ushei na 80 na Martin Odegaard dakika ya 71.
  Kwa ushindi huo Washika Bunduki wanafikisha pointi 60 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 25, wakati Everton inabaki na pointi zake 21 za mechi 25 pia nafasi ya 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL ‘IS ON FIRE’, EVERTON YAFA 4-0 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top